Hamidu Hassan Bobali |
Jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama cha Wananchi CUF JUVICUF linatarajia kufanya zoezi la usafi Katika eneo la makao makuu ya Chama hicho Buguruni jijini Daresalaam.
Kwan mujibu taarifa iliyotolewa na kiongozi umoja huo taifa Hamidu Hassan Bobali (Mb) na Mwenyekiti wa JUVICUF Taifa.
Shughuli hiyo itafanyika siku ya jumapili ambapo vijana wote wata kutana Buguruni paliko makao makuu ya cha wananchi CUF.
Vilevile JUVICUF imeomba vijana wote wapenda maendeleo jijini Dar es Salaam na maeneo ya jirani wafike Kwa umoja ili kutekeleza azma yao hiyo.
Hata hivyo Hamidu Hassan mwenyekiti wa JUVICUF aliacha wito kwa kuwataka vijana kutotumika vibaya katika shughuli za ujenzi wa Chama na taifa kwaujumla.
“tunatoa wito kwa baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakirubuniwa na kutumika na vibaraka wa ccm, kuacha mara moja kutaka kuivuruga cuf. Mafanikio tuliyoyapata mwaka 2015 yanahitaji kulindwa na kuongezeka mara mbili zaidi 2020 . Wenye jukumu la kufanikisha hilo Si wengine ni sisi vijana. Tuache tabia ya kutumika kirahisi rahisi ili kufanikisha maslahi ya watu wachache. Maslahi ya taifa letu linatutegemea zaidi vijana kuliko kundi lolote lile. Tusipoamua kutumia vizuri vichwa vyetu katika kufikiri, vibaraka watatumia nguvu zetu katika kuhofisha juhudi za ukombozi wa taifa letu.
Nape akiwa anaongea na wanahabari hivi karibuni aliwahi kunukuu usemi wa mwanazuoni mmoja usemao " there is nothing , nothing to fear than fear itself ".”
No comments:
Post a Comment