Katibu wa BAWACHA Taifa Bi Grace Tendega akihutubia wakazi wa Arusha Mjini waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliondaliwa na BAWACHA Wilaya ya Arusha Mjini na kufanyika katika eneo la Soko Kuu Arusha, Kata ya Kati. Kabla ya hapo Mh Tendega alikuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu wa BAraza hilo kwa Wilaya ya Arusha Mjini ambapo viongozi wa baraza hilo kwa Kata zote za Arusha Mjini pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanawake watokanao na CHADEMA.
Katika mkutano wa Soko Kuu, Tendega aliwahimiza wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi na kuhamasishana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu baadae mwaka huu na kutimiza kile wanachoamini kuwa ni kushinda uchaguzi huo na kukamata dola.
Katika mkutano wa Soko Kuu, Tendega aliwahimiza wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi na kuhamasishana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi mkuu baadae mwaka huu na kutimiza kile wanachoamini kuwa ni kushinda uchaguzi huo na kukamata dola.
Akisisitiza jambo
Grace Tendega akiagana na wana Arusha mkutanoni hapo kwa ishara ya kukunja ngumi na kuitikia salamu ya "people's…power"
Katibu wa CHADEMA Kata ya Kati ulipofanyika mkutano huo Bw Hassan Noor akipozi kwa picha na viongozi wanamama mara baada ya mkutano
Meza kuu mkutanoni
Msafara wa Katibu wa BAWACHA Taifa Mh grace Tendega akiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa wakiwasili katika eneo la stand ya 'mabasi luxury' Levolosi ambapo kulikuwa na zoezi la uzinduzi wa tawi la CHADEMA na yeye ndiye aliyepewa heshima ya kufanya uzinduzi huo rasmi.
Maandalizi ya uzinduzi wa tawi kwa kupandisha bendera. Wajumbe wametulia kusikiliza maelekezo
Mh Grace tendega akipandisha bendera kumaanisha uzinduzi rasmi wa tawi
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akitoa neno kwa wanatawi na mashuhuda wengine wa tukio hilo la uzinduzi
Grace Tendega akizungumza mara baada ya uzinduzi rasmi
Mwananchi akiwa amemganda Mh tendega wakati akiondoka

0 Comments:
Post a Comment