WASHITAKIWA KWA KUICHAGUA CHADEMA

 
 
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji cha Nyamihundu Kata ya Nzihi kimewakamata vijana wanne kwa tuhuma za kukipigia kura Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hayo yalibahinishwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (Bavicha), John Heche, alipozungumza na waandishi wa habari.

Aliwataja vijana hao kuwa ni Petro Ngoro, Saba Kabongo na Samsi Ngojela wote wa Kijiji cha Nyamihundu na  James Futa, mkazi wa Tosamaganga, Kata ya Kalenga.
 
SOURCE TANZANIA DAIMA

0 Comments:

Post a Comment