TAMICO KUMBURUZA KORTINI DC MONGELA


CHAMA cha Wafanyakazi  Migodini,Nishati,Ujenzi na Kazi  (TAMICO),
Kanda ya Kaskazini, imempa siku saba Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John
Mongela kufuta kauli yake ya kuita chama hicho ni matapeli, lasivyo
atamburuza  Mahakamani.
Katibu wa TAMICO, Kanda ya Kaskazini, Anasimbo  Nico  Lema,
akizungumzia sakata hilo jana na waandishi wa habari ofisini kwa
Jijini Arusha, alisema Mkuu huyo ameingilia majukumu ya vyama vya
wafanyakazi ambayo yeye hayamuhusu kisheria.
"Huyu Mkuu wa Wialaya Arusha anaingilia kazi za kutetea wafanyakazi,
wakati hajulikani kisheria nab ado anamfuata mwajiri ambaye mwekezaji
mzawa anamwambia asitutambue sisi ni matapeli, kwakweli akanushe kauli
hii kw akuitisha kikao baina yangu na mwajiri nay eye la sivyo
namburuza mahakamani baada ya siku saba,"alisema.
Alisema chanzo cha hayo kutokea yeye kama katibu aliletewa mashitaka
na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Jiangai Geo Corporation  Ltd,
ambayo kwa sasa inafanya ujenzi wa dampo Ungalimited kuwa,
inawanyanyasa wafanyakazi wake kwa kuwalipa ujira mdogo wa shilingi
5,500 kwa siku badala ya 12,500 kwa siku kama sheria ya kazi
inavyosema.
"Mimi nilivyopata malalamiko haya nilikwenda kw amwajiri ambaye ni
mchina wa kampuni hii na nikaongea naye alikubali tufanye kikao Machi
10 mwaka huu pia alikubali kwa maandishi, lakini ilipofika siku
yenyewe alikataa na kudai mimi tapeli hawezi kufanya kikao na tapeli
na Mkuu wa Wilaya akaniita mimi tapeli mbele ya mwekezaji na
kunifukuza ofisini kwake,"alisema.
Lema alisema kampuni hiyo kimsingi inanyanyasa wafanyakazi kwa sababu
wapo vijana wenye kufanya kazi zaidi ya miaka saba lakini hadi sasa
hawajaajiriwa nab ado wanakatwa malipo yao bila sababu ya msingi.
Alisema wapo wafanyakazi  43 wa kampuni hiyo, lakini miongoni mwao
mmoja ambaye ni Miraji Mkombozi, ameachishw akazi kinyemela Machi 9
mwaka huu kwa madai ya kuhamasisha wenzake kukaa kikao cha kuzungumza
madai yao na kumlipa shilingi 25,000.
"Kijana huyu amefanya kazi miaka mitatu, lakini anaachishw ana kulipwa
shilingi hizi haziwezi kumtosheleza kitu chochote na kinyume cha
sheria, sasa nikitaka kukaa meza moja kama sheria inavyonielekeza,
Mkuu wa Wilaya anakataza na kuvunga kikao kuwa mimi tapeli,"alisema.
Naye Mwenyekiti wa tawi la TAMICO kwenye kampuni hiyo, Said Ramadhani
Ally, alisema  wao wanamgogoro na mwajiri wao, ambaye amemwachisha
kazi mwenzao bila sabahbu za msingi, huku wafanyakazi wengine
wakilipwa ujira mdogo usiendana na mikataba ya kazi walivyokubaliana.
"Tunaomba serikali iangalie suala hili, lakini pia sisi tunategemea
serikali itusaidie sana, ila chakushangaza tumeshuhudia Mkuu wa Wilaya
akimfukuza Katibu wetu wa TAMICO kwenye kikao kwa madai ni tapeli,
hivi tufafika wapi na sisi tutafanyaje tumebaki njia panda,"alisema.
Mkuu wa Wilaya  ya Arusha, John Mongela, akizungumza na Nipashe kwa
njia ya simu ya kiganjani, alikiri kumwambia Katibu wa TAMICO ni
tapeli, kutokana na tabia yake ya kwenda kwa wachina kuomba fedha za
kujikimu, badala ya kushughulikia matatizo ya msingi ya wafanyakazi.
"Kweli  huyu bwana  ni tapeli na nimemwambia hivyo juzi na alikimbia
ofisini kwangu la sivyo ningemweka pingu na akija tu tena pale ofisini
kwangu namweka pingu maana ni tapeli,"alisisitiza.
Mongela alisema kimsingi anafahamu baadhi ya makampuni ya Wachina nchi
nzima ni wanyanyasaji wa wafanyakazi, lakini vyama vya wafanyakazi
badala ya kuwatetea, wanawageuza mabomba ya kujipatia kipato kwa
kuwakocho wafanyakazi kuleta vurugu kwa waajiri wao, kisha nao
wanajitokeza na kutaka posho ili kutuliza hali hiyo.
"Sasa vijana wanapolipuka tu kudai maslahi yao na huku wanapewa
shinikizo badala ya kuwatatulia kero zao ni hatari, lakini mimi tayari
nimeshughulikia suala lao na kweli wana hoja za msingi na ndani ya
siku tatu watalipwa stahiki zao,"alisema Mongela.

0 Comments:

Post a Comment