Sunday, March 16, 2014

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014

Taarifa ya Katibu wa Bunge Maalum kwa Vyombo vya Habari

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

BUNGE MAALUM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014

 Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dododma kesho kwa ratiba ifuatayo:

Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na  kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa. Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa  kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa 2:00  asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.

Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha  Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.

Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.

Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum  na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum.

 Atakayeipata taarifa hii amjulishe mwenzake.

 

Imetolewa na Ofisi ya

KATIBU WA BUNGE MAALUM

No comments:

Post a Comment