MAELEKEZO YA JUMLA: MUDA 30 DK.
• Mtihani huu ufanywe na kila mtanzania mwenye kiwango chochote cha ufahamu wa elimu ya uraia na kiwango chochote cha ufahamu na uzalendo kwa Tanzania.
• Ukifanya mtihani huu utakuwa umeingie kwenye historia ya kufanya mtihani mmoja na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na wote wanaotetea serikali mbili.
• Kuibilizia ni kosa la kiuzalendo, isipokuwa kuuliza usipo elewa ni tunu ya kizalendo
• Wimbo wowote wa kizalendo na hotuba za Mwalimu Nyerere na Karume zinaweza kutumika kama rejea (Reference) pale mtahaniwa atakapo ona inafaa.
• Chagua jibu moja na sahihi kwa kila swali, hakuna swali litakalo kuwa na majibu mawili.
• Matumizi ya simu za mkononi na vipeperushi vya aina ya vibuti ni kosa la kizalendo.
• Mtihani huu utakuwa wa maswali kumi (10) tu, na jibu maswali yote kama una kitu na si kinyama mwitu
• ili uweze kufaulu mtihani huu lazima 99.8% ya majibu yako yafanane, Msahihishaji ni Sheikh Farid akishirikiana na Mch CHRISTOPHER MTIKILLA
MASWALI.
1. Umeshasikia au kusoma popote kwenye historia kuhusiana na nchi iliyokuwa inaitwa Tanganyika?
A. Ndio
B. Hapana
C. Sijui
2. Nchi hiyo (Tanganyika) ilipata uhuru wake na kuwa nchi yenye mamlaka kamili mwaka
A. 1961
B. 1964
C. Sijui
3. Je nchi hiyo ilikuwa na rais wake, jeshi lake, sarafu yake, wimbo wake wa Taifa na tunu zote za kuwa nchi kamili?
A. Ndio
B. Hapana
C. Sijui
4. Nchi inayoitwa Tanganyika iliungana na nchi nyingine iliyokuwa inaitwa jamhuri ya watu wa Zanzibar na kuunda jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka.
A. 1964
B. 1961
C. Hakuna jibu sahihi
5. Je nchi hizo zilipo ungana (Tanganyika na Zanzibar) Moja ilikufa na kupoteza asili yake huku nyingine ikibaki na asili na tunu zake kama nchi?
A. Ndio
B. Hapana
C. Sijui
6. Je ilikuwa ni sahihi kwa nchi moja kufa na kupoteza asili yake huku nchi nyingine ikibaki na hadhi ya kuwa nchi na mamlaka yake na bado ukaitwa muungano?
A. Ndio
B. Hapana
C. Hakuna jibu sahihi
7. Kwa kuwa Zanzibar imeendelea kubaki kuwa nchi kamili na Tanganyika kufa, ni sahihi kusema Zanzibar imeimeza Tanganyika? Yaani sawa na kusema Dagaa imemeza Sangara?
A. Ndio
B. Hapana
C. Sijui
8. Kwa muungano wa nchi mbili, ni sahihi nchi moja kuwepo na nchi nyingine kuuliwa kwa hila wakati muungano niwa nchi mbili huku baadhi ya viongozi kuona kinyaa kuizungumzia nchi waliyo iua?
A. Ndio
B. Hapana
C. Dhambi isiyo na msamaha
9. Ili muungano uwe na maana ya kuitwa muungano wa nchi mbili, je itakuwa sahihi kuirudisha na kuifufua Tanganyika?
A. Ndio
B. Hapana
C. Sijui
10. Je inawezekana kuwa na muungano wa nchi mbili lakini moja isitambulike na hivyo kupoteza kwa makusudi historia ya nchi nyingine
A. Hapana
B. Ndio
C. Sijui
Baada ya kumaliza kujibu maswali hayo hapo juu tafakuri chokonozi kwa faida ya nyumbani ni kujiuliza, Je dagaa anaweza kummeza Sangara (Yaani Zanzibar kuimeza Tanganyika) na je, ni sahihi kwa mwenyekiti wa CCM kumeza maoni ya tume ya Warioba iliyokusanya maoni Tanzania nzima (Yaani ni sahihi Papa kumezwa na Kambale)?!
Wasalimie Watanganyika wenzako.
No comments:
Post a Comment