ASKARI
Polisi F 5264, PC Sabato, (37) ameuawa kwa kupigwa jiwe kichwani na mtuhumiwa,
Njoke Ole Kilimbi, (34) wakati
akimepeleka mahabusu kwenye gereza la Mkoa, Kisongo.
Tukio hilo
limetokea JUMATANO WIKI HII mchana eneo karibu na hilo baada ya kushuka kwenye
gari la abiria walilotumia ambapo walitembea umbali mfupi kabla ya kukutwa na
dhahama hiyo ambapo aliokolewa na waendesha bodaboda.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo
alisema kuwa askari huyo alifariki juzi majira ya tano usiku wakati akipatiwa
matibabu kwenye hospitali ya Mount Meru.
No comments:
Post a Comment