KADA wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM)
wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi, Edward Lowassa anadaiwa kutumia kigezo cha udini kutaka kuungwa
mkono kwenye harakati za kukimbilia Ikulu jambo linalohatarisha amani ya nchi.
Aidha Rais Jakaya Kikwete ametakiwa
kuweka hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya madawa ya kulevya ambayo
aliwahi kulitangazia Taifa kuwa anayo vinginevyo itakuwa ni vigumu kuondoa
mashaka kuwa si mshirika wao.
Hayo yalisemwa juzi na Mwanasheria
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Tundu Lissu na wakati akimnadi
mgombea udiwani wa kata ya Sombetini, Ally Bananga kwenye viwanja vya Ngusero.
Lissu alisema kuwa baada ya Lowassa kuona
hana sifa za uongozi kutokana na kuwa si muadilifu wala safi kulingana na
tuhuma za ufisadi zinazomwandama ameamua kukimbilia makanisani akiwashawishi
viongozi wa dini wamuuunge mkono kwa kigezo cha kuwa ni Mkristo mwenzao.
“Kuna makada wengine wa CCM nao
wanazunguka huko misikitini wakisema hii ni zamu yetu sisi Waislam hivyo
anashawishi wamchague kwa kigezo cha Uislam tu .Hawa watu wanasahau dini si
kigezo wala sifa ya uongozi tuwakataeni, sijui wanalipeleka wapi hili Taifa
zaidi wanatutafutia machafuko hawatufai wote hawa,” alisema Lissu.
Akizungumzia muswada wa madiliko ya
katiba, Lissu alisema kuwa katiba inasema kuwa nchi ni moja lakini kwa
sasa kuna Maamiri Jeshi wawili ambao mmoja ni Mwenyekiti wa CCM, Kikwete na
mwingine ni Makamu wake, Dk Mohamed Shein jambo alilosema kuwa ni hatari sana
hasa ikitokea wakitofautiana na kupishana kauli ilihali wote wanamajeshi.
JUHUDI ZA KUMPATA LOWASSA KUZUNGUMZIA MADAI HAYA ZILIGONGA MWAMBA BAADA YA SIMU YAKE YA KIGANJANI KUPOKEWA NA MTU MWINGINE AKIDAI MBUNGE HUYO WA MONDULI YUKO KIKAONI AMBAPO ALITAKA APIGIWE BAADA YA SAA MOJA
ALIPOPIGIWA TENA SIMU HIYO ILIITA BILA KUPOKELEWA
0 Comments:
Post a Comment