WAENDESHA bodaboda wa jiji la Arusha wa memuomba
mkuu wa jeshi la polisi (IGP),Ernest Mangu kuwaondoa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani (RTO) , mkaguzi wa polisi Daud mshana , na koplo Peter , ambao
wamekuwa ni wasumbufu na vinara wa kuomba rushwa huku RTO, akidaiwa kukataa kuwasikiliza na badala yake huwa anawafukuza wanaofika ofisini
kwake .
Mwenyekiti wa umoja wa waendesha pikipiki (UWAPA), Godlight Rugemalila, alisema lengo la maandamano yao ya siku mbili ni
kupinga vitendo vya jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani cha
kuwabambikizia makosa na kuwatoza faini kubwa ,sanjari na kuwaomba
rushwa .
kero
nyingine ni pale wanapokamatwa na polisi pikipiki zao zinafungwa
minyororo (Chain) na kupelekwa polisi kikosi cha usalama barabarani na
kupata usumbufu kuzikomboa licha ya kulipa faini huzungushwa mpaka watoe
rushwa .
Wamesema
katika risala yao kuwa kero kubwa kuliko zote ni mkuu wa kikosi cha
usalama bara
barani, R.T.O,Marison Makyoma, ambae amekuwa akiwalazimisha kutoa rushwa na
kutumia ubabe na vitisho na pia amefuta vituo vya maegesho ya pikipiki
vilivyoidhinishwa na halmashauri ya jiji katika maeneo mengi .
Wametaka kuwepo dawati la boda boda kwenye kituo cha
polisi ili kuweza kutatua matatizo yao na hivyo kuwaondolea usumbufu
anaoupata sasa.
Wamesema boda boda ni mkombozi kwa wananchi zimetoa ajira kwa wengi na hivyo kupunguza uhalifu .
Wamesema boda boda ni mkombozi kwa wananchi zimetoa ajira kwa wengi na hivyo kupunguza uhalifu .
Wamesema
katika jiji la Arusha kuna vituo 144 vya boda boda na vingine tayari
vina uongozi na vingine vipo katika mchakato wa kukamilisha uongozi .
Katika
maandamano hayo waendesha boda boda walikuwa na mabango yenye ujumbe
mbalimbali ikiwemo,
"Tumechoshwa kufanywa ATM na jeshi la polisi, IGP ,Ernest mangu , muondoe R.T.O ni majanga Arusha,Hatutoki nasi ni watanzania tumechoshwa kugeuzwa kuwa mashine za ATM, haya ni majanga
"Tumechoshwa kufanywa ATM na jeshi la polisi, IGP ,Ernest mangu , muondoe R.T.O ni majanga Arusha,Hatutoki nasi ni watanzania tumechoshwa kugeuzwa kuwa mashine za ATM, haya ni majanga
Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa wilaya ya Arusha, John Mongela ametoa amri ya kusitisha kwa wiki mbili oporesheni ya ukaguzi na ukamataji pikipiki hizo za kubeba abiria.
Alisema ametoa muda huo ili kuwawezesha wamiliki na madereva kukamisha taratibu na sheria za usalama barabarani ikiwemo madereva kuwa na leseni pamoja na kuwa na kofia maalum ya kuendesha vyombo hicvyo vya moto.
Hata hivyo operesheni ya kusaka pikipiki zote
zinazojihusisha katika matukio ya uhalifu inaendelea bila kikomo katika
maeneo yote ya wilaya ya Arusha lengo ni kudumuisha usalama katika
vijiwe mbalimbali vya boda boda..
Mongela, amewaeleza waendesha pikipiki jijini Arusha kupitia Umoja
wao waendesha pikipiki (UWAPA) kwenye uwanja wa mpira wa Sheik Amri
Abeid Januari 15, mwaka huu.
Mongela amewaagiza waendesha bodaboda hao wawe na uongozi kila
kijiwe ili kuwatambua waendesha pikipiki ambao sio waaminifu
wanajihusisha na vitendo vya uhalifu ambao wanawaharibia sifa yao ya kutoa
huduma ya usafiri.
Mongela,
amba pia ni mlezi wa waendesha boda boda jijini Arusha,
amewataka wasikubali kutoa rushwa kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani badala yake wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria na watoe taarifa kwake au kwa mkuu wa
polisi wa mkoa (RPC) na wilaya (OCD) pindi akiombwa rushwa.
Amewataka
wawe na vitambulisho , kuvaa vijamba koti (vizibao) maalumu ,sanjari na
kuwa na kofia mbili moja kwa ajili ya abiria na kuhakikisha abiria
wanavaa kofia hizo.
0 Comments:
Post a Comment