TANAPA KUENDESHWA KWA MFUMO WA KIJESHI ILI KUDHIBITI UJANGILI





Katika kukabiliana na vitendo vya ujangili vinavyoendelea kushika kasi ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) litaendeshwa katika mfumo wa jeshi-usu katika siku chache zijazo ambapo watumishi wake watalazimika kupitia katika mafunzo maalum ya kijeshi.


Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya askari wapya 96 walioajiriwa na TANAPA na kuhudhuria mafunzo ya miezi minne katika Hifadhi ya Taifa Katavi mwishoni mwa wiki.



Kijazi alisema kuwa TANAPA imeanzisha utaratibu mpya ambapo sasa askari wanaoajiriwa na shirika kutoka katika Vyuo vya Wanyamapori vya Mweka na Pasiansi pamoja na wale wa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa watalazimika kupitia mafunzo maalum yanayoandaliwa na shirika kwa ajili ya kuwawezesha waajiriwa wapya kufahamu mazingira halisi ya utendaji kazi katika eneo la uhifadhi katika maeneo ya Hifadhi za Taifa.








 Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo Sajini Taji Simon Mbunda akipokea zawadi yake iliyotolewa na wahitimu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA



Sehemu ya askari waliohitimu mafunzo ya miezi minne kwa askari waajiriwa wapya wakimsikiliza mgeni rasmi.


Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Katavi Ignas Gara akiongea wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo.




0 Comments:

Post a Comment