Saturday, October 13, 2012

CHATANDA ANURURIKA KUPIGWA UCHAGUZI WA UV CCM


KATIBU wa Chama Cha mapinduzi (CCM),  mkoani hapa,Mary Chatanda amenusurika kupokea kipigo baada ya kutuhumiwa kuvuruga uchaguzi wa mkoa wa  jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UV CCM) akidaiwa kutaka kumpitisha mmoja wa wagombea,Dk. Harold Adamson.

Tukio hilo lilitokea oktoba 10, mwaka huu majira ya saa tisa alasiri wakati Chatanda ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo kuamuru zoezi la uchaguzi huo lirudiwe baada ya kuwa ulishafanyika kwa madai kwamba idadi ya wajumbe kutoka wilaya za Monduli na Arumeru haikuwa sahihi.

Hali hiyo ililazimu Jeshi la polisi na maafisa usalama wa Taifa kuingilia kati kuhakikisha hali ya amani inarejea ambapo polisi hao waliletwa kwenye eneo hilo na gari aina ya land rover ambalo ubavuni limeandikwa OCD lenye namba za usajili PT 0746 ambao waliamua kuwaamrisha waandishi kutoka nje ya lango kuu ili wasione kilichokuwa kikiendelea ndani ya ukumbi huo.

Hata hivyo vurugu hizo zinazohusishwa na makundi hasimu ya  Urais 2015 ndani ya CCM kwani tokea chaguzi hizo zianze mkoani hapa kuanzia ngazi ya wilaya hali hiyo ilikuwa ikijidhihirisha wazi ambapo mara  baada ya hali kutulia uchaguzi huo ulirudiwa huku ulinzi ukiwa umeimarishwa na milango ya kuelekea eneo hilo ikiwa imefungwa.
 Awali kabla ya tafrani hiyo kutokea hali ya upepo kwenye zoezi hilo la upigaji kura lililoanza majira ya saa sita mchana kwa nafasi hiyo ya mwenyekiti ilionyesha  huenda mgombea,Robinson Meitenyiku akaibuka na ushindi wa kishindo.  

Chatanda aliwaamuru wajumbe wote  wa mkutano huo watoke nje ya ukumbi kwa madai kwamba kuna baadhi yao kutoka wilaya za Meru na Monduli walizidi kitendo wajumbe hao wakukubaliana nacho.

Hata hivyo wajumbe hao walitii na kutoka nje ya ukumbi wa uchaguzi huku wakipaza sauti kwamba katibu huyo analengo la kuvuruga uchaguzi huo kwa kuwa anataka kumpitisha mgombea ambaye ni chaguo lake na kundi lake ,Dk Adamson.

Aidha wajumbe kutoka wilayani Monduli walionekana kupandisha jazba wakimtaka Chatanda kuendesha kikao kwa kuzingatia sheria huku  wakitishia kumchapa ndani ya ukumbi huo jambo ambalo hawakuweza kulitekeleza kutokana na Jeshi la polisi kuwasili eneo hilo hivyo uchaguzi huo kuendelea chini ya ulinzi mkali.

Hata hivyo wajumbe hao walikuwa wakilalamika  kuwa wakati wa uchaguzi wa awali walipinga hatua ya Chatanda kukaa karibu na sanduku la kupigia kura kwa madai kuwa licha ya kuwa msimamizi lakini taratibu hazimruhusu kufanya hivyo huku wengine wakidai kuwa walipokuwa wakipita karibu yake alikuwa akiwashawishi wampigie kura mgombea wake.

Kwa upande wake katibu mwenezi wa kata ya Mbuguni, Joshua Mbwana alisema nje ya ukumbi kuwa watu wanaolipwa mshahara ndani ya CCM ndiyo mara zote wamekuwa wakivuruga mambo ndani ya chama hicho tawala kwani wanajua hata wakiharibu na vyama vya upinzani vikaendelea kuchukua majimbo mishahara yao iko palepale.

Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo aliyeongea kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini alisema kuwa mara baada ya kuamua kurudia uchaguzi huo Chatanda alijaribu kuibua hoja mpya kuwa kuna baadhi ya wajumbe umri wao ni mkubwa jambo ambalo walilipinga kwani wajumbe hao walipitishwa na wilaya zao hivyo yeye hana uhalali wa kuwapinga.

Mpaka majira ya saa 12 jioni wanachama wa chama hicho pamoja na wajumbe ambao walikuwa wameshapiga kura walionekana kujitenga kwenye makundi mawili moja lango la nyuma la kuingia kwenye jengo la CCM mkoa na wengine kwenye lango la mbele

No comments:

Post a Comment