MAANDAMANO YA WAANDISHI YATIKISA NCHI NZIMA


Wanahabari waandamana nchi nzima kulaani mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi


Kutoka viwanja vya Jangwani, Dar es Salaa: Katibu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena, akihutubia waandishi wa habari walioandamana kulaani mauaji yaliyofanywa na polisi dhidi ya mwandishi Daudi Mwangosi mkoani Iringa hivi karibuni.
Mhariri Mkuu wa Channel Ten, Dinnah Chahali akiwa amezungukwa na waandishi wa habari wakati wa maandamano ya wanahabari jijini Dar es Salaam kupinga kuuawa kwa mwakilishi wa kituo hicho mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.
 Huko Moshi Polisi wa usalama barabarani waliamua kubeba jukumu la wanahabari kwa kupiga picha za matukio mbalimbali. Uandishi wa habari ni Mzuri bwana.
 Viongozi wa KPC nao walishiriki vyema Maandamano hayo mjini Moshi.
 Waandishi wa habari wa Jijini Dar es Salaam wakiandamana hii leo.
Waziri wa mambo ya Ndani, Dk. Nchimbi nae alivamia hapa na wanahabari wa jijini Dar es Salaam kumkataa na kuamua kuondolewa na vijana wake kwa kuhofia usalama wa ke dhidi ya Camera na Kalamu. 

kwa hisani ya Father Kidevu

0 Comments:

Post a Comment