RUFAA YA LEMA YAPANGIWA JAJI ANAYETUHUMIWA NA LISSU HAKIDHI VIGEZO


RUFAA  ya kupinga kuvuliwa ubunge ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless  Lema, (CHADEMA) imepangwa kusikilizwa Septemba 20, mwaka huu mbele ya  majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na
Salmu Massati.


Kwa mujibu taarifa  za kikao cha mahakama ya rufaa cha Arusha rufaa hiyo namba 47/2012 iiliyofunguliwa na  Lema akipinga uamuzi uliotengua ubunge wake kufuatia shauri lililofunguliwa mahakama kuu kanda ya Arusha na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo.

Kikao hicho cha mahakama ya rufaa kinatarajia kusikiliza shauri hilo kwa siku moja ambapo baada ya hapo kitapanga tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.


Awali Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro aliwasilisha kwenye mahakama ya rufaa hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na mahakama kuu kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu. 

Kwenye baadhi ya madai hayo,Lema  aliiomba Mahakama ya rufaa kutengua uamuzi wa mahakama kuu, uliomtengua Ubunge wake huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa jimbo la Arusha Mjini.

Aidha aliitaka mahakama hiyo ya juu iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye mahakama kuu kanda ya Arusha.

Katika madai mengine Lema anamlalamikia Jaji, Gabriel Rwakibarila aliyesikiliza kesi hiyo kwenye mahakama kuu kanda ya Arusha kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa jaji alikosea  wakati alipoamua kuwa mpiga kura yoyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

0 Comments:

Post a Comment