CHAMA cha Wanunuzi wa Kahawa Tanzania (TCBA), kimewajia juu wabunge wanaomshinikiza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, atangaze kupiga marufuku ununuzi wa kahawa mbivu.
Katibu Mkuu wa Chama hicho, Eric Ng’maryo, aliwaambia waandishi wa habari mjini Moshi jana kuwa, Waziri Mkuu anapaswa kushauriwa vizuri na wasaidizi wake, kwa vile kutoa tamko kama hilo ni kinyume cha sheria.
“Nimefuatilia kwa karibu hoja zilizoibuliwa bungeni na waheshimiwa wabunge wawili kutoka mkoa wa Mbeya, lakini namsihi Waziri Mkuu kuwa suala hilo liangaliwe kisheria na si kisiasa,” alisema Ng’maryo.
Kwa mujibu wa Ng’maro, biashara ya kahawa nchini inatawaliwa na Sheria ya Tasnia ya Kahawa ya Mwaka 2001 na kanuni zake, hivyo kama zinatakiwa kutenguliwa, lazima utaratibu ufuatwe.
“Kanuni za biashara ya kahawa mbivu, iliridhiwa na wadau wa kahawa katika mkutano uliofanyika Morogoro, Aprili mwaka huu na hii ndio jukwaa sahihi la maamuzi,” alisema.
Alisema uamuzi wa wadau ambao ni pamoja na wanunuzi binafsi, wakulima wadogo na wakubwa na wasafirishaji nje ya nchi, ndio unaompa nguvu ya kisheria Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, kutunga kanuni.
Alisema uamuzi wa wadau wa kutaka kuendelea kwa biashara ya kahawa mbivu, ulitungiwa kanuni na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na kanuni hizo, zilipata nguvu ya kisheria Mei 25, mwaka huu.
Alisema kanuni hizo, zilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali kwa G.N namba 187 la Mei, 25 na kuhoji “Waziri anahusikaje na kanuni hizi…haya ni makubaliano ya wadau, tusipotoshe umma”.
Kuhusu suala la ununuzi wa kahawa mbivu kuwa linamnyonya mkulima, Ng’maryo alisema hiyo ni dhana potofu na propaganda chafu ili kuua ushindani wa kibiashara mkoani Mbeya.
“Ili kupata kilo moja ya kahawa ya maganda, utahitaji kilo tano za kahawa mbivu na kama kilo moja ya kahawa mbivu ni Sh 1,000, kilo tano itakuwa Sh 5,000, mkulima ananyonywaje?” alihoji.
Aliwataka wanaopotosha suala hilo kutokana na maslahi binafsi, waache kuwayumbisha wakulima ambao ndiyo wenye uamuzi wa wapi wakauze kahawa yao.
Wakichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu unaoendelea bungeni, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na wa Rungwe Magharibi, David Mwakyusa (CCM), walipinga biashara hiyo.

0 Comments:
Post a Comment