Friday, June 1, 2012

UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA 47 WA BENKI YA MAENDELEO AFRIKA (AfDB)






 Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete zungumza kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya washiriki 2400 toka nchi wanachama barani Afrika, Asia na Ulaya
  
Alitaka  miundombinu barani Afrika iboreshwe ili kuwezesha a sekta ya utalii  kufanya vizuri jambo litakaloongeza  pato kubwa akitolea mfano nchi ya Tanzania kwa kusema kuwa kwa sasa pato kubwa linatoka katika madini na huku utalii ikiwa inashika nafasi ya pili kwa kuingiza pato kubwa



 Rais wa Ivory Cost, Dk. Alassane Ouattara akiongea kwenye mkutano huo ambapo alishukuru kwa uamuzi wa kurudisha makao makuu ya AfDB kwenye mji mkuu wa nchi yake Abidjan baada ya kuhama kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na machafuko yaliyokuwa nchini mwake
 Mwakilishi wa mfalme wa Morocco, akizungumza kwenye mkutano huo akishukuru kwa nchi yake kupewa fursa ya kuandaa mkutano mkuu ujao wa AfDB





Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka akiongea kwenye mkutano huo  alisema kuwa  hazina kubwa iliyofichika kwa Afrika, sio mafuta, gesi au madini bali ni vijana .
 
Alizitaka serikali za Afrika kusimamia vema raslimali zilizopo ili ziweze kuleta maendeleo kwa nchi hizo, vinginevyo, raslimali hizo zitakuwa laana.
 
Alisema AfDB imedhamiria kuwekeza katika sekta ya miundombinu ingawa pengo la mahitaji ya fedha na mahitaji halisi ya uwekezaji katika sekta hiyo ni kubwa.

Waziri wa fedha, William Mgimwa akimnong'oneza jambo Rais Jakaya Kikwete



Sehemu ya washiriki wa mkutano huo ambao agenda yake kubwa ilikuwa ni uboreshaji wa miundombinu



 

Sehemu ya washiriki 


No comments:

Post a Comment