NCHI za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya kudhibiti masuala ya
rushwa, kila mwaka zinapoteza zaidi ya USD bilioni 148 kwa kutoroshwa na kufichwa nchi za ughaibuni.
Tanzania imepewa heshima ya ujenzi wa Ofisi ya Bodi ya Kupambana
na Rushwa katika Nchi za Umoja wa Afrika (AU) zitakazojengwa Jijini
Arusha mwaka huu wa fedha .
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini, (TAKUKURU),Dk,Edward Hoseah wakati
akifungua mkutano wa siku tano ulioshirikisha wakuu wa
Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi mbalimbali za
Afrika na Wataalam kutoka Taasisi zisizo za Kiserikali .
Alisema kuwa mkutano huo unajadili changamoto mbalimbali za hali ya
rushwa katika nchi za Afrika ambazo zitaenda kujadiliwa
kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaotarajia kufanyika nchini
Ethiopia hivi karibuni pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo kupitia hali ya
Rushwa katika nchi za AU.
Aliongeza kuwa Jiji la Arusha limechaguliwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa katika Nchi za AU na tayari serikali
imeshatenga eneo la ujenzi wa ofisi hiyo na mwaka huu wa fedha
serikali imeshatenga fungu kwaajili ya ujenzi huu ingawa hakutaka
kutaja ni kiasi gani .
Mjumbe wa Bodi hiyo ,Alberic Kacou alisema matokeo ya rushwa
katika nchi nyingi za Afrika yanaleta umaskini,ukosekanaji wa huduma
bora za jamii pamoja na kupunguza kasi ya uchumi na maendeleo na
kukemea rushwa kwenye chaguzi mbalimbali kwani kiongozi anayepita kwa
rushwa anapoteza uaminifu katika uongozi

0 Comments:
Post a Comment