UKATILI dhidi ya wanawake nchini Tanzania unaendelea baada ya mwanamke mjamzito, Neisisiri Mokoroo (25) kuuawa kwa kuchapwa na fimbo na mume wake, Kapaito Naanjarati kwa madai kuwa ujauzito aliokuwa nao ni wa mwanaume mwingine.
Tukio hilo limetokea 6, mwaka huu wakati walipokuwa shambani wakikata nyasi kwenye kijiji cha Olkeijulongishu wilayani Longido ambapo mwanaume huyo alitoweka baada ya kuona mke wake amefariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Liberatus Sabas amesethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wanamtafuta mwanaume huyo ambapo mwili wa marehemu, Mokoroo umehifadhiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Longido.
No comments:
Post a Comment