Mtendaji Mkuu wa ICF, Omary Issa amesema kuwa ICF imesaidia kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni nchini Rwanda ambapo kwa sasa humchukua mtu siku 2 kusajili biashara tofauti na awali ambapo ilikuwa wakitumia mpaka siku 16 huku gharama zikipungua kutoka dola za Marekani 433 mpaka 25.
Issa alisema kuwa taasisi yake katika kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika kwa urahisi na ufanisi zaidi imesaidia kuboresha mfumo wa mahakama nchini Zambia kwenye mahakama 3 na kutoa mafunzo kwa majaji wapya 14 huku nchini Sierra Leone wakifanikiwa kuboresha mfumo wa mahakama ambapo kwa sasa huchukua miezi miwili tokea kufungua kesi za biashara na kupata uamuzi ambapo awali ilikuwa inatumia mpaka miaka sita .
alisema kuwa taasisi hiyo inashirikiana na TRA na Jeshi la polisi nchini kuboresha utoaji huduma kwa kuhakikisha bidhaa zinazopita nchini (transit goods) kwenda nchi jirani ya Rwanda zinasafirishwa kwa usalama na haraka kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Rusumo kwenye mpaka wa nchi hizo hivyo kupunguza gharama za usafirishaji.
afisa wa TRA, Alexander Buchafwe,
MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imeanzisha mfumo wa kieletroniki wa kufuatilia magari ya mizigo (ECTS) ambao utasaidia kukabiliana na udanganyifu wa baadhi ya wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kuingiza mali nchini kwa madai kuwa zinapita kuelekea nje ya nchi.
Aidha mfumo huo ambao utawezesha magari hayo kufuatiliwa moja kwa moja kutoka kwenye ofisi za TRA huku vifaa hivyo vikutunza taarifa utasaidia kuondoa vizuizi vya kukagua kodi kwenye barabara ambavyo vilikuwa vikionekana kuwa kero kubwa kwa wenye malori hasa kutokana na uwingi wake.
Hayo yalisemwa na afisa wa TRA, Alexander Buchafwe, alipokuwa akitoa maelezo kwenye banda ya taasisi za serikali za nchi za Afrika zilizonufaika na Taasisi ya kuboresha uwekezaji Afrika (ICF) ambayo inafanya mkutano wake pili mkubwa wa kimataifa kwenye hoteli ya Naura Spring.
Alisema kuwa mfumo huo ulizinduliwa rasmi Machi 12, mwaka huu ambapo wamewapa wamiliki wote wa magari ya mizigo muda wa miezi mitatu wawe wamefunga vifaa hivyo kutoka kwa makampuni sita waliothibitishwa na TRA kwa ajili ya kufanya kazi ya kuuza na kufunga vifaa hivyo.




0 Comments:
Post a Comment